26 Juni 2025 - 19:43
Sayyid Ali Khamenei: "Utawala wa Kizayuni haukufikiria kamwe kupokea mashambulizi kama haya kutoka kwa Jamhuri ya Kiislamu".

Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu - Leo akihutubia Taifa la Iran, ametoa ufafanuzi mzuri mno wa matukio yalivyojiri, na kauli imara za kutia moyo kwa wananchi wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran, ambazo kwa hakika zimeonyesha mshikamano wa kitaifa, ujasiri, na kukataa kuachia madikteta au nguvu za kigeni na kibeberu kutawala na kuidhibiti Kijeshi Mashariki ya Kati. Pia, kauli za Kiongozi huyu imara na mwenye busara na hekima ya hali ya juu, zinaonyesha msimamo wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran katika kukabiliana na mashambulizi ya nje, na kutotetereka katika suala zima la kuifyekelea mbali mikono ya adui yeyote yenye nia ovu dhidi ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran.

Shirika la Habari la Kimataifa la Ahlul-Bayt (as) -ABNA- Sayyid Ali Khamenei, Kiongozi Mkuu wa Mapinduzi ya Kiislamu, leo hii amehutubia Taifa la Iran na Kuzungumzia vita vya kulazimishwa dhidi ya Iran vilivyoanzishwa na Israel na vikadumu kwa muda wa  Siku 12.

Sayyid Ali Khamenei: "Utawala wa Kizayuni haukufikiria kamwe kupokea mashambulizi kama haya kutoka kwa Jamhuri ya Kiislamu".

Ametoa ufafanuzi mzuri mno wa matukio yalivyojiri, na kauli imara za kutia moyo kwa wananchi wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran, ambazo kwa hakika zimeonyesha mshikamano wa kitaifa, ujasiri, na kukataa kuachia madikteta au nguvu za kigeni na kibeberu kutawala na kuidhibiti Kijeshi Mashariki ya Kati. 

Pia, kauli za Kiongozi huyu imara na mwenye busara na hekima ya hali ya juu, zinaonyesha msimamo wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran katika kukabiliana na mashambulizi ya nje, na kutotetereka katika suala zima la kuifyekelea mbali mikono ya adui yeyote yenye nia ovu dhidi ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran.
_
Miongoni mwa mambo muhimu aliyosema Ayatollah Sayyid Ali Khamenei, Kiongozi Mkuu wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran (Leo hii):

1_Mashambulizi ya kiuadui dhidi ya Iran yatakuwa na gharama kubwa sana.

2_Utawala wa Kizayuni haukufikiria kamwe kupokea mashambulizi kama haya kutoka kwa Jamhuri ya Kiislamu.

3_Vikosi vyetu vya Kijeshi vimeweza kupenya na kupita kwa urahisi mno kwenye mfumo wa ulinzi wa adui na kuvitwanga vituo (shabaha) vingi katika moyo wa adui (ndani kabisa katika maeneo muhimu sana ya adui).

4_Rais wa Marekani anafanya kuonyesha ukubwa wa tukio lililotokea kwamba haijawahi kutokea, na hili linaakisi haja ya Marekani ya kuanzisha madai kama haya.

5_Rais wa Marekani anaficha ukweli halisi wa kile kilichotokea kwa kujificha nyuma ya madai kama hayo.

6_Kufikia kwa Jamhuri ya Kiislamu katika vituo muhimu vya Marekani kama vile kambi ya Al-Udeid Nchini Qatar, si jambo la kawaida.

7_Shambulizi la uadui la Marekani dhidi ya vituo vyetu vya nyuklia halikufikia malengo yoyote yale kwa maadui.

8_Wananchi wa Iran walikusanyika kwa umoja wao bila kugawanyika, na wote walikuwa wakibeba kauli moja inayounga mkono vikosi vya Kijeshi.

9_Marekani inapojaribu kupunguza ukali wa pigo la Iran dhidi ya kambi ya Al-Udeid ina lengo la kuficha ukweli halisi, na siku zijazo zitatuonyesha kiwango halisi cha hasara iliyoingia kwa maadui.

10_Iran, yenye kumiliki nguvu za kijeshi, azma, na mshikamano wa kitaifa, haitakubali unyonge wala kujisalimisha kama inavyosema siku zote.

11_Lengo la Marekani kila wakati limekuwa ni kutaka kuilazimisha Iran isalimu amri, jambo ambalo halikusemwa na yeyote katika marais wa Marekani wa zamani, kinyume na rais huyu wa sasa.

12_Udhalilishaji ulioelekezwa na Marekani kwa Wananchi wa Iran hautatimia kamwe, na watu wetu ni watu adhimu, na Taifa letu ni Taifa imara, na ustaarabu wetu umejaa historia ndefu.

13_Watu wetu ni washindi, na wenye izza na heshima, na wataendelea kuwa hivyo kwa himidi za Mwenyezi Mungu na nguvu Zake.

Tags

Your Comment

You are replying to: .
captcha